69 – Bishr bin Muhammad ametuhadithia: ´Abdullaah ametukhabarisha: Mu´aawiyah bin Abiy Muzarrid ametukhabarisha: Nimemsikia ami yangu Sa´iyd bin Yasaar akisimulia kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Allaah aliumba viumbe mpaka alipomaliza kuwaumba, akakiambia kizazi: ”Hii ndio nafasi yako inayokaliwa na yule ambaye anaomba kinga Yako dhidi ya ukataji.” Akasema: ”Ndio.” Je, huridhii Nimuunge yule mwenye kukuunga na Nimkate yule mwenye kukukata? Kikasema: ”Ndio, ee Mola.” Ndipo akasema: ”Unakubaliwa jambo hilo.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Someni kama mnataka:

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ

”Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? – hao ndio wamewalaani na Allaah akawafanya viziwi na akawapofua macho yao.”[1]

70 – ´Abdullaah bin Yuusuf ametuhadithia: al-Layth ametuhadithia, kutoka kwa ´Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab: Nimemsikia ´Urwah akisema: ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akarejea kwa mkewe Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akitetemeka. Akaingia ndani ya kusema: Kisha baada ya muda akasema: “Nifunikeni! Nifunikeni!” Alipotulia, akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Nimechelea juu ya nafsi yangu.” Khadiyjah akasema: ”Pata bishara njema. Naapa kwa Allaah! Allaah hatokutweza. Kwani hakika wewe unaongea kweli, unaunga kizazi, unamkirimu mgeni, unawasaidia wenye kukosa, unabeba mazito [ya watu] na unasaidia katika shida mbalimbali.” Hivyo Khadiyjah akampeleka kwa Waraqah bin Nawfal bin Asad. Alikuwa ni mzee na kipofu ambaye ameingia katika unaswara na alikuwa akisoma injiyl kwa kiarabu. Khadiyjah akamwambia: ”Msikize nini anachotaka kusema mtoto wa ndugu yako.” Waraqah akamwambia: ”Kipi unachoona, ee mtoto wa ndugu yangu?” Akamweleza yale aliyoyaona. Ndipo Waraqah akasema: “Hii ni Naamuus ambayo ilikuwa ikimjilia Muusa. Laiti ningelikuwa ni kijana mwenye nguvu na hai pindi watapokufukuza watu wako.” Akasema: ”Je, watanifukuza?” Akasema: “Ndio. Hakuna mtu yeyote aliyekuja na mfano wa ulichokuja nacho isipokuwa aliudhiwa.” Kama nitakuwa naishi katika kipindi chako, basi nitakunusuru nusura yenye nguvu.”

71 – Sulaymaan bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-´Alaa’ na wengineo wametuhadithia kwamba wamemsikia Bilaal bin Sa´d, kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Ee Mtume wa Allaah, nini nitakuwa kwa khaliyfah wa baada yako?” Akasema: ”Mfano wa kile kilichonitokea, muda wa kuwa atakuwa mwadilifu katika kuhukumu, akigawa kati na kati na akiwarehemu jamaa. Yule anayefanya kingine basi hatokani nami nami sitokani naye.”

Bi maana anachokusudia ni utiifu katika kumtii Allaah na maasi katika kumuasi Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 47:22-23

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 160-163
  • Imechapishwa: 21/01/2025