62 – Aadam bin Abiy Iyaas ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia: ´Uyaynah bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisimulia kutoka kwa Abu Bakrah: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna dhambi ambayo kuna uwezekano mkubwa Allaah akamuharakishia mwenye nayo adhabu yake duniani pamoja na yale Aliyomwandalia huko Aakhirah, kama kukata kizazi na dhuluma.”
63 – Umayyah bin Bistwaam ametuhadithia: Yaziyd bin Zuray´ ametuhadithia, kutoka kwa al-´Alaa’, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia:
”Bwana mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Mimi nina jamaa ambao ninawaunga na wao wananikata. Nawafanyia upole na wao wananifanyia ujinga. Nawafanyia wema na wao wananifanyia mabaya.” Akasema: ”Ikiwa mambo ni kama hivo unavosema, basi ni kama vile unawalisha majivu. Utaendelea kuwa na msaidizi kutoka kwa Allaah muda wa kuwa utaendelea katika hali hiyo.”
64 – Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, al-Hasan bin ´Amr na Fitwr, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Anayeunga sio mwenye kulipiza wema. Lakini muungaji ni yule ambaye, wakati kizazi kinapokatwa basi yeye anakiunga.”
Sufyaan amesema:
”al-A´mash hakuisimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Fitwr na al-Hasan wameipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
65 – Maalik bin Ismaa´iyl ametuhadithia: ´Iysaa bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Awsajah, kutoka kwa al-Baraa’ (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:
”Bedui mmoja alikuja na kusema: ”Ee Nabii wa Allaah! Nifunze kitendo kitachoniingiza Peponi.” Akasema: ”Hata kama umefupisha lakini umeuliza swali pana. Komboa nafsi huru na wacha mtumwa huru.” Akasema: ”Hayo si ni kitu kimoja?” Akasema: ”Kukomboa nafsi huru ni wewe kuiacha nafsi huru. Kuacha mtumwa huru ni wewe kumsaidia mtumwa na kutoa kondoo jike na ngawira kumpa jamaa mwenye kudhulumu. Usipoweza chochote katika hayo, basi uamrishe mema na ukataze maovu. Usipoweza chochote katika hayo, basi usizungumze chochote isipokuwa chenye kheri.”
66 – Abul-Yamaan ametuhadithia: Shu´ayb ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy: ´Urwah bin az-Zubayr amenikhabarisha kwamba Hakiym bin Hizaam amemukhabarisha kwamba alisema kumwambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Katika kipindi kabla ya kuja Uislamu nilikuwa nafanya ´ibaadah kama vile kuunga kizazi, kuacha watumwa huru na kutoa swadaqah; je, nalipwa thawabu kwa hayo?” Haakim akasimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Umesilimu juu ya zile kheri zilizotangulia.”
67 – ´Abdur-Rahmaan bin Shariyk ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa Bukayr bin ´Abdillaah bin al-Ashajj, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Maymuunah (Radhiya Allaahu ´anhaa), mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Alimwacha kijakazi wake huru. Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoingia kwake, akamweleza jambo hilo. Ndipo akasema: ”Allaah amekulipa thawabu, lakini ungeliwapa wajomba zako basi malipo yako yangelikuwa makubwa zaidi.”
67 – ´Abdur-Rahmaan bin Shariyk ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa Bukayr bin ´Abdillaah bin al-Ashajj, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, ambaye amesema:
”Maymuun (Radhiya Allaahu ´anhaa), mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alimwacha huru kijakazi wake. Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoingia kwake, akamweleza jambo hilo. Adipo akasema: ”Allaah amekulipa thawabu, lakini ungeliwapa wajomba zako basi malipo yako yangelikuwa makubwa zaidi.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 154-159
- Imechapishwa: 21/01/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 154-159
Imechapishwa: 21/01/2025
https://firqatunnajia.com/27-kukata-udugu-na-dhuluma/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)