276. Ni ipi hukumu kwa wanawake kutembelea kaburi la Mtume?

Swali 276: Ni ipi hukumu kwa wanawake kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Vile ninavoona ni kwamba kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kama makaburi mengine. Haijuzu kwa mwanamke kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ambavo haifai kuyatembelea makaburi mengine, kutokana na kuenea kwa Hadiyth:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyafanya ni mahali pa kuswalia na kuyaweka mataa.”[1]

[1] Abu Daawuud (3236), at-Tirmidhiy (320), an-Nasaa’iy (2043) na Ahmad (2030). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (225).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/316-317)
  • Imechapishwa: 28/05/2022