Imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ee Allaah! Yule ambaye nitamtawalisha katika watu wa Ummah wangu jambo lolote ambapo akawafanyia upole basi Nawe mfanyie upole. Na yule ambaye nitamtawalisha katika watu wa Ummah wangu jambo lolote ambapo akawafanyia ugumu basi Nawe mfanyie ugumu.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Ee Allaah! Unapaswa kufanya upole katika ulinganizi wako na usiwafanyie ugumu watu, usiwakimbize mbali na dini, usiwakimbize kutokana na ukali, ujinga wako wala kwa mtindo wako wa kijeuri, unaoudhi na wenye kudhuru. Ni lazima uwe mpole, mwenye kusubiri, mwenye uongozi mzuri na mwenye maneno laini ili uathiri moyo wa ndugu yako na uathiri moyo wa yule anayelinganiwa. Aidha kuwa hivyo ili afarijike na ulinganizi wako na alainike nao, aathirike nao, akusifu kwao na akushukuru kwao. Kuhusu ususuwavu ni kitu kinachokimbiza watu mbali na hakiwasogezi karibu, kinafarikisha na hakikusanyi.

[1] Muslim (1828).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 14/06/2023