Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Lakini ukimuelekea Allaah (Ta´ala) na ukasikiliza hoja na ubainifu Wake, hutokhofu na wala hutohuzunika.

إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا

“Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.” (04:76)

MAELEZO

Hapa (Rahimahu Allaah) anachotaka ni kumtia moyo yule mwenye kumuelekea Allaah (Ta´ala) na akaitambua haki, ya kwamba asiogope hoja za watu wa batili. Kwa sababu ni hoja nyonge na ni njama za shaytwaan. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا

“Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 04/11/2023