Imaam Abul-Ma´aaliy al-Juwayniy amesema:

“Wanazuoni wametofautiana kuhusu haya maandiko ya dhahiri. Wako ambao wameona yanatakiwa kupindishwa maana na wakalazimiana na mfumo huo juu ya Aayah za Qur-aan na Sunnah Swahiyh za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maimaamu wa Salaf wameonelea kujiepusha na kupindisha maana, kuyapitisha kwa dhahiri yake na kumtegemezea maana zake Mola. Kile tunachokichagua kama maoni na tunamwabudu Allaah kwacho kama ‘Aqiydah ni kuwafuata Salaf wa ummah. Dalili ya hakika ya kiuteremsho juu ya hilo ni kwamba maafikiano ya ummah ni hoja inayofuatwa. Kwa hiyo endapo upindishaji maana wa maandiko haya ya dhahiri ingekuwa inafaa au yenye kuheshimiwa, basi ingetegemewa kuwa walivipa umuhimu kuliko hata matawi ya Shari´ah. Kama zama za Maswahaba na wanafunzi wao zilipita bila kupekua maana zake, basi hiyo ndiyo njia inayofuatwa.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Abuu Ismaa’iyl al-Answariy amesema:

“Mlango unaozungumzia kuthibitisha kuwa Allaah yuko juu ya ‘Arshi Yake juu ya mbingu ya saba hali ya kuwa mbali na viumbe Wake, kutokana na Qur-aan na Sunnah… Kuna mapokezi mbalimbali yanayosema kuwa Allaah yuko juu ya mbingu ya saba juu ya ‘Arshi Yake kwa nafsi Yake na anatazama namna mnavyotenda. Ujuzi Wake, uwezo Wake, kusikia Kwake, kuona Kwake na rehema Yake viko kila mahali.”

Imaam Abu Muhammad al-Baghawiy amesema:

”Allaah (Subhaanah) amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[2]

al-Kalbiy na Muqaatil amesema:

”Kwa maana akathibiti.”

Abu ´Ubaydah amesema:

”Kwa maana akapanda.”

Mu´tazilah wamepindisha maana kulingana kwamba ni kutawala, ilihali Ahlus-Sunnah wanasema kuwa kulingana juu ya ´Arshi ni sifa ya Allaah (Ta´ala)  ambayo haitakiwi kufanyiwa namna na kwamba ni wajibu kuiamini.”[3]

[1] al-´Aqiydah an-Nidhwaamiyyah, uk. 34

[2] 7:54

[3] Ma´aalim-ut-Tanziyl (2/165).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 29/12/2025