Swali: Je, kuna kipambanuzi katika du´aa ya Qunuut katika Ramadhaan? Nikikusudia ni kwamba yale anayoomba imamu katika usiku mmoja ndani ya Ramadhaan mara moja au mara mbili ima katika lile kumi la mwanzo, kumi la pili au kumi la mwisho? Je, yalikuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake au ni kitu gani kinachofanyika Madiynah, Makkah, mji mkuu wa misikiti na kadhalika ar-Riyaadh ikiwa ni sahihi kama inafanyika ndani ya Ramadhaan mara moja au mara mbili? Nataraji uwawekee wazi ummah katika kila msikiti ni mamoja msikiti huo ni mkubwa au mdogo?

Jibu: Du´aa ya Qunuut katika Witr imependekezwa kutokana na Hadiyth ya al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinifunza maneno nitakayosema katika Witr:

اللهم اهدِنا فيمَن هديت وعافنا فيمن عافيت وتولنا فيمن توليت وبارك لنا فيما أعطيت وقِنا شر ما قضيت [ف]انك تقضي ولا يقضى عليك [و]اٍنه لا يذل مَن واليت [ولا يعزُ من عاديت]تباركت ربنا وتعاليت لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, nisalimishe pamoja na Uliowasalimisha na nilinde pamoja na Uliowalinda. Tubariki katika kile Ulichotupa na tukinge na shari ya Uliyotuhukumia. Kwani hakika Wewe unahukumu wala huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemlinda, na wala hatukuki Uliyemfanya adui. Umebarikika, ee Mola wetu, na umetukuka. Hakuna mahali pa kuokoka kwengine isipokuwa Kwako.”[1]

Wameipokea wapokezi wa Sunan.

Endapo muislamu baadhi ya nyakati ataacha du´aa hii na mara nyingine akaiomba ni sawa. Ni mamoja ni ndani ya Ramadhaan au miezi mingine.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

[1] Ahmad (1727), Abu Daawuud (1425) na an-Nasaa’iy (1745). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Qiyaam Ramadhwaan, uk. 31-32”.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 20/04/2022