26. Uumbaji wa Allaah ni kitu kimoja, neno Lake ni kitu kingine

Allaah ametofautisha kati ya amri na viumbe Wake; hakuwaita viumbe Wake kuwa amri Yake. Amesema:

أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ

”Tanabahi! Ni Vyake pekee uumbaji na amri.”[1]

Aliposema kuwa viumbe ni Wake, kukaingia viumbe wote. Kisha Akataja ambacho hakikuumbwa na kusema:

وَالْأَمْرُ

”… na amri.”

Amri Yake ndio maneno Yake. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu, kutokana na maneno Yake kuwa yenye kuumbwa!

Amesemea tena:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ

“Hakika Sisi tumeiteremsha katika usiku uliobarikiwa – hakika Sisi daima ni Wenye kuonya [watu] – katika [usiku] huo hupambanuliwa kila jambo la hekima.”[2]

Kisha akasema kuhusu Qur-aan:

أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا

”… ni amri inayotoka Kwetu.”[3]

Kisha akasema:

لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ

”Amri ni ya Allaah pekee kabla na baada.”[4]

Bi maana Allaah ndiye Mwenye neno kabla na baada ya kuumba. Allaah anaumba na anaamrisha – na maneno Yake sio uumbaji Wake. Amesema:

ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ

”Hiyo ni amri ya Allaah amekuteremshieni.”[5]

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ

”… mpaka ilipokuja amri Yetu na maji yakachimbuka kwa nguvu kutoka katika tanuri… ”[6][7]

[1] 7:54

[2] 44:3-4

[3] 44:5

[4] 30:4

[5] 65:5

[6] 11:40

[7] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 22/04/2024