1 – Miongoni mwa shubuha zao ni baadhi yao kutumia dalili kwa kule kufikia baadhi ya malengo yao kwenye makaburi. Kama wanavosema kwamba kuna mtu fulani ameomba kwenye kaburi la fulani, aliita kwa jina la Shaykh fulani au walii fulani ambapo akafikia mahitajio yake. Jibu ni kwamba mshirikina kufikia baadhi ya malengo yake si dalili yenye kuonyesha kufaa ile shirki anayofanya. Kile alichofikia kunaweza kuwa kumekutana na mipango na makadirio ya Allaah na huku akifikiria kuwa kumetokamana na maombi ya Shaykh au walii huyo kama ambavo kunaweza kuwa kunatokamna na kuvutwa polepole au kupewa mtihani. Kwa hali yoyote haifahamishi kujuzu kuombwa asiyekuwa Allaah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 42-43
- Imechapishwa: 02/04/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)