ad-Duwaysh amesema:
“Bali Dr Rabiy´ al-Madkhaliy ameenda mbali zaidi ambapo amefadhilisha wafuasi wengi wa Zaydiyyah na watu wao wa kawaida pamoja na wafuasi wa Ibaadhiyyah na watu wao wa kawaida juu ya wafuasi wa madhehebu mane. Amesema:
“Wako wafuasi wa madhehebu ya Zaydiyyah na watu wao wa kawaida na wafuasi wa Ibaadhiyyah na watu wao wa kawaida ambao wako karibu zaidi na maumbile na Tawhiyd kuliko wafuasi wengi wa madhehebu mane. Wako mbali na shirki, ukhurafi, kuyaabudu makaburi na Suufiyyah kuliko walivyo wafuasi wengi wa madhehebu mane.”[1]
Jambo la kwanza Shaykh Rabiy´ amewafadhilisha hao waliotajwa hapo juu ya wafuasi wa madhehebu mane kwa upande mmoja, nao si Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ambayo ndio msingi.
Jambo la pili wanachuoni wote wanajua kuwa ufadhilishaji wa sehemu haupelekei ufadhilishaji katika kila kitu. Kwa mfano kusema kwamba mtu fulani ni mjuzi wa kiarabu zaidi kuliko mwingine, haina maana pia kwamba ni mjuzi wa kila kitu kuliko huyo mwingine.
Jambo la tatu ni kwamba haimaanishi Saudi Arabia. Kwa sababu Saudi Arabia hakuna shirki wala kuyaabudu makaburi waziwazi kama ilivyo katika jamii zengine za Kiislamu ambao wanasema kuwa wanafuata madhehebu mane. Huko shirki na kuyaabudu makaburi ni mambo yako waziwazi. Makuba na makaburi yanaabudiwa badala ya Allaah. Hapa kunapata kubainika tuhuma za batili za mtu huyu dhidi ya Salafiyyuun na kuwatuhumu mambo wasiyokuwa nayo.
[1] Ahl-ul-Hadiyth hum-ut-Twaa-ifah al-Mansuurah, uk. 2
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 50-51
- Imechapishwa: 04/12/2018
ad-Duwaysh amesema:
“Bali Dr Rabiy´ al-Madkhaliy ameenda mbali zaidi ambapo amefadhilisha wafuasi wengi wa Zaydiyyah na watu wao wa kawaida pamoja na wafuasi wa Ibaadhiyyah na watu wao wa kawaida juu ya wafuasi wa madhehebu mane. Amesema:
“Wako wafuasi wa madhehebu ya Zaydiyyah na watu wao wa kawaida na wafuasi wa Ibaadhiyyah na watu wao wa kawaida ambao wako karibu zaidi na maumbile na Tawhiyd kuliko wafuasi wengi wa madhehebu mane. Wako mbali na shirki, ukhurafi, kuyaabudu makaburi na Suufiyyah kuliko walivyo wafuasi wengi wa madhehebu mane.”[1]
Jambo la kwanza Shaykh Rabiy´ amewafadhilisha hao waliotajwa hapo juu ya wafuasi wa madhehebu mane kwa upande mmoja, nao si Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ambayo ndio msingi.
Jambo la pili wanachuoni wote wanajua kuwa ufadhilishaji wa sehemu haupelekei ufadhilishaji katika kila kitu. Kwa mfano kusema kwamba mtu fulani ni mjuzi wa kiarabu zaidi kuliko mwingine, haina maana pia kwamba ni mjuzi wa kila kitu kuliko huyo mwingine.
Jambo la tatu ni kwamba haimaanishi Saudi Arabia. Kwa sababu Saudi Arabia hakuna shirki wala kuyaabudu makaburi waziwazi kama ilivyo katika jamii zengine za Kiislamu ambao wanasema kuwa wanafuata madhehebu mane. Huko shirki na kuyaabudu makaburi ni mambo yako waziwazi. Makuba na makaburi yanaabudiwa badala ya Allaah. Hapa kunapata kubainika tuhuma za batili za mtu huyu dhidi ya Salafiyyuun na kuwatuhumu mambo wasiyokuwa nayo.
[1] Ahl-ul-Hadiyth hum-ut-Twaa-ifah al-Mansuurah, uk. 2
Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 50-51
Imechapishwa: 04/12/2018
https://firqatunnajia.com/26-mtazamo-wa-rabiy-al-madkhaliy-juu-ya-wafuasi-wa-madehebu-mane/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)