56 – Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia: Sulaymaan bin Kathiyr ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mnajua nini ninachoona? Mimi naona fitina zikiyazunguka majumba yenu.”
57 – al-Fadhwl bin Dukayn ametuhadithia: Ibn ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa Usaamah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mnajua nini ninachoona? Mimi naona fitina zikiyazunguka majumba yenu kama mvua.”
58 – ´Abdaan ametuhadithia: ´Abdullaah ametuhadithia: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa Kurz bin ´Alqamah, ambaye amesema:
”Bedui mmoja alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Je, Uislamu una mwisho?” Akasema: ”Ndio. Hakuna watu wa nyumba yoyote ya kiarabu au isiyokuwa ya kiarabu ambayo Allaah ataitakia kheri isipokuwa atawaingizia Uislamu. Kisha kutazuka fitina kana kwamba ni viza.” Bedui yule akasema: ”Kamwe.” Akasema: ”Bila shaka, naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Halafu mnarudi huko, kama nyoka walioinuliwa, ambapo mnaanza kukatana vichwa nyinyi kwa nyinyi.”
59 – ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia: al-Layth amenihadithia: Naafiy´ amenihadithia, kutoka kwa ´Abdullaah, aliyeeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema hali ya kuwa ameelekea mashariki:
”Fitina itatokea hapa, fitina itatokea hapa, kule ambako kutazuka pembe ya shaytwaan.”
60 – Sa´iyd bin Muhammad al-Jirmiy ametuhadithia: Ya´quub bin Ibraahiym ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Swaalih: Naafiy´ ametuhadithia kwamba ´Abdullaah amemukhabarisha mfano wake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
61 – Khaalid bin Makhlad ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia: ´Abdullaah bin Diynaar ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye amesema:
”Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiashiria mashariki na akisema: ”Fitina itatokea hapa. Fitina itatokea kule ambako itazuka pembe ya shaytwaan.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 151-153
- Imechapishwa: 20/01/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 151-153
Imechapishwa: 20/01/2025
https://firqatunnajia.com/26-majaribio-ya-mvua/