50 – Ibraahiym bin al-Mundhir ametuhadithia: Ma´n ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Jubayr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Nawwaas bin Swam´aan al-Answaariy ambaye ameeleza kwamba:

”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya wema na dhambi. Akasema: ”Wema ni tabia njema, na dhambi ni yale yanayokukereketa nafsini mwako na ukachelea watu wasije kuyajua.”

51 – Abul-Yamaan ametuhadithia: Shu´ayb ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy: Saalim amenihadithia, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema juu ya mimbari:

”Hapana shaka kwamba fitina itatokea hapa, ambapo kutazuka pembe ya shaytwaan.”

Akaashiria Magharibi.

52 – ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia: al-Layth amenihadithia: ´Uqayl amenihadithia, kutoka kwa Ibn Shihaab, Saalim bin ´Abdillaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum) amenikhabarisha, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama akiwakhutubia watu na akasema: ”Fitina itatokea hapa, ambapo kutazuka pembe ya shaytwaan.” Bi maana Mashariki.”

53 – al-Humaydiy ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr bin ´Alqamah ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin ´Abdir-Rahmaan bin Haatwib, kutoka kwa ´Abdullaah bin az-Zubayr: az-Zubayr amesema:

”Wakati kuliposhuka:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”[1]

az-Zubayr alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Tutazozana, baada ya mizozo tuliokuwa nayo duniani?” Akasema: ”Ndio.” Ndipo nikasema: ”Mambo ni mazito.”

54 – Muhammad bin ´Ubaydillaah Abu Thaabit al-Madaniy ametuhadithia: ´Umar bin Twalhah al-Waqqaasiy ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr, kutoka kwa Yahyaa bin ´Abdir-Rahmaan: Nimemsikia ´Abdullaah bin az-Zubayr akisema:

”Wakati kuliposhuka:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”

az-Zubayr alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Je, yale madhambi tuliyofanya duniani yatakaririwa?” Akasema: ”Ndio.” Yatakaririwa kwenu, mpaka kila mwenye haki apewe haki yake.” az-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: ”Naapa kwa Allaah! Mambo ni mazito.”

Hammaad bin Salamah amepokea mfano wa hayo, kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa al-Hasan: az-Zubayr amesema… Shaddaad bin Sa´iyd amepokea mfano wa hayo, kutoka kwa Ghaylaan, kutoka kwa Mutwarrif: az-Zubayr amesema… Matamshi yao ni yenye kukaribiana. Hata hivyo ile ya kwanza ndio Hadiyth Swahiyh zaidi.

55 – Abur-Rabiy´ Sulaymaan bin Daawuud ametuhadithia: Ya´quub al-Qummiy ametuhadithia: Ja´far – Ibn Abiyl-Mughiyrah – ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye amesema:

”Wakati kuliposhuka:

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

”Halafu hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtazozana.”

hatukujua tafsiri yake. Wakati kulipotokea fitina, tukasema: ”Haya ndio yale ambayo Mola wetu ametuahidi kuzozana kwayo.”

[1] 39:31

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 146-150
  • Imechapishwa: 20/01/2025