26. Kuzidisha katika du´aa ya Qunuut ya Witr

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anazidisha juu ya Qunuut baadhi ya du´aa? Je, inafaa au haifai? Kwa sababu nimesoma katika kitabu “Swifatu Swalaat-in-Nabiy” cha Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ambapo amesema:

“Miongoni mwa Sunnah ni kuwa hatuzidishi katika Qunuut ya Witr swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walifanya hivo.”

Mimi nasikia, khaswa katika mwezi wa Ramadhaan, ya kwamba baadhi ya ndugu wanazidisha baadhi ya du´aa katika Qunuut ya Witr.

Jibu: Imethibiti katika Hadiyth ya al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomfunza Qunuut katika Witr. Katika “al-Musnad” ya Ahmad, Sunan ya Abu Daawuud, ya at-Tirmidhiy, ya an-Nasaa´iy, ya Ibn Maajah na wengineo ya kwamba yeye (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinifunza maneno nitakayosema katika Witr:

اللهم اهدِنا فيمَن هديت وعافنا فيمن عافيت وتولنا فيمن توليت وبارك لنا فيما أعطيت وقِنا شر ما قضيت [ف]انك تقضي ولا يقضى عليك [و]اٍنه لا يذل مَن واليت [ولا يعزُ من عاديت]تباركت ربنا وتعاليت لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, nisalimishe pamoja na Uliowasalimisha na nilinde pamoja na Uliowalinda. Tubariki katika kile Ulichotupa na tukinge na shari ya Uliyotuhukumia. Kwani hakika Wewe unahukumu wala huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemlinda, na wala hatukuki Uliyemfanya adui. Umebarikika, ee Mola wetu, na umetukuka. Hakuna mahali pa kuokoka kwengine isipokuwa Kwako.”[1]

at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth hii ni nzuri. Hatujui kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Qunuut chochote ambacho ni kizuri zaidi kuliko hiki.”

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema mwishoni mwa Witr yake:

اللهم إني أعوذ برضاك من سخطك, وبمعافاتك من عقوبتك، وأعوذ بك منك، لا أحصي ثناءً عليك, أنت كما أثنيت على نفسك

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa ridhaa Yako kutokamana na hasira Zako, msamaha Wako kutokamana na adhabu Yako na naomba ulinzi Kwako kutokamana na Wewe. Siwezi kukusifu vile Unavostahiki Wewe ni kama vile Ulivyojisifu Mwenyewe.”[2]

Mwombaji akiomba katika zile du´aa fupifupi zenye maana pana na khaswa miongoni mwa zile du´aa zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo litafaa. Kwa sababu ni miongoni mwa aina ya du´aa ya Qunuut na isitoshe ni mahali pa kuomba du´aa. Hivo ndivo walivosema kikosi cha wanazuoni.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

[1] Ahmad (1727), Abu Daawuud (1425) na an-Nasaa’iy (1745). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Qiyaam Ramadhwaan, uk. 31-32”.

[2] Wameipokea watano.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 27-29
  • Imechapishwa: 18/04/2022