26. Komeka na kula kabla ya kushiba

132 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: ´Abdullaah bin Swadaqah al-Qaysiy ametuhadithia: ´Iysaa bin Zaadhaan ametuhadithia:

”Siku moja Ziyaad al-Qaysiy alinambia tukiwa katika nyumba ya watawala:

Patwa na njaa – kwani hakika njaa ni katika ngawira za mchaji

yule mwenye kuhisi njaa kwa kipindi kirefu atakuja kushiba siku moja

Naapa kwa Allaah! Nikazunduka na kuelewa anachokusudia. Nikasema: ”Namtoa fidia baba yangu kwako! Hutomuona bwana wako akila mchana maishani.” Akasema: ”Hicho ndicho nimekitaka kutoka kwako. Wataalamu wanapaswa kushughulikia vipi chakula wakati wa mchana?” Hapana, naapa kwa Allaah. Yote yanahusiana na malezi ya kiroho na utoshelevu mpaka ifike amri ya Allaah. Matumbo yatakuwa yamepangwa kwa ajili ya kumtamani Allaah na juu ya kukutana Naye.”

133 – Muhammad ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz bin Salmaan amenihadithia: Nimemsikia ´Iysaa bin Zaadhaan akisema kwa sauti ya huzuni:

Lazimiana na riziki ya wafanya ´ibaadah na jambo lao na uchache wa chakula

– kwani wewe unafanya kwa ajili ya Allaah

Utibu moyo wako mzima kwa glasi moja

– na fanya haraka, kwani jambo haliepukiki

´Iysaa alikuwa ni miongoni mwa watu wanaotosheka na walichonacho.

134 – Muhammad amenihadithia: ´Abdul-Jabbaar bin Abiy Naswr amenihadithia: Amatullaah bint Abiy Naswr amenihadithia:

”Siku moja Salamah al-Aswaariy alimwambia kijana mmoja ambaye alikaa naye kitambo kirefu:

Hakikisha unakuwa na njaa kipindi kirefu, kwa sababu

kukaa na njaa muda mrefu kutakufurahisha siku ya Qiyaamah

135 – Muhammad amesema: Yaziyd bin ´Abdillaah bin Sukayn al-Faarisiy amenihadithia: Rafiki yangu mmoja mfanya ´ibaadah amenihadithia:

”Jioni moja baada ya kula futari nilizidisha kiwango, nililemewa kwenda kuswali. Nikaota namna jinsi wanawake wananifanyia maombolezo, nikawaambia: ”Mnanifanyia maombolezo ilihali bado niko hai.” Wakanambia: ”Bali wewe ni katika wafu. Je, hivi hujui ya kuwa kula kwa wingi kunaidhoofisha miili, kuua moyo na kumfanya mtu akawa kama mwenye kulala?” Nikasema: ”Nifanye nini sasa?” Wakasema: ”Kiache chakula ilihali unakitamani. Ni salama zaidi kwa mwili wako wakati wa uzima wako na kali zaidi kwa hamu yako ya chakula wakati inaporudi.”

136 – Muhammad amenihadithia: as-Swalt bin Hakiym ametuhadithia: Nimemsikia ´Abdullaah bin Marzuuq akisema:

”Hakuna kitu kinachopambana na shari kama njaa.”

Akasema: “Abu ´Abdir-Rahmaan al-´Umariy az-Zaahid akasema: ”Unafikiri inajumuishaje?” Akasema: ”Inajumuisha usishibe hata siku moja.” Akasema: ”Ni vipi mtu aliye duniani ataweza jambo hilo?” ´Abdullaah akasema: ”Ni jambo jepesi lilioje, ee Abu ´Abdir-Rahmaan, kwa mawalii Wake!” Yule ambaye Allaah amemuwafikisha katika kumtii, hali mpaka akashiba. Hiyo ndio njaa yenye kudumu.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 91-94
  • Imechapishwa: 24/07/2023