26. Imamu anajikakama kisomo katika Tarawiyh kwa kutaka kulainisha nyoyo za watu

Swali 26: Baadhi ya maimamu wa misikiti hujaribu kuzilainisha nyoyo za watu na kuwaathiri kwa kubadilisha mtindo wa sauti zao. Baadhi ya nyakati wanafanya hivo katikati ya swalah ya Tarawiyh na katika du´aa ya Qunuut. Nimewasikia baadhi ya watu wakikemea jambo hilo. Unaseamje juu ya hilo?

Jibu: Kile ninachoona ni kwamba ikiwa kitendo hichi ni kwa mujibu wa mpaka wa Shari´ah pasi na kuchupa mpaka basi hakuna ubaya wala neno. Abu Muusa al-Ash´ariy alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ningelijua kuwa unasikiliza kisomo changu basi ningekurembea zaidi.”

Baadhi ya watu wakiziremba sauti zao na wakazitumia kwa njia ya kutaka kuzilainisha nyoyo za watu,  basi sioni kuwa kuna makosa. Lakini kuchupa mpaka katika jambo hili kwa njia ya kwamba havuki neno hata moja ndani ya Qur-aan isipokuwa anafanya hivo alivyoeleza katika swali, basi naona kuwa itakuwa ni kupetuka mpaka ambako hakutakiwi. Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 26
  • Imechapishwa: 20/04/2021