25. Imamu wa msikiti anaigiliza kisomo cha Qur-aan cha wasomaji wengine

Swali 25: Baadhi ya maimamu wa misikiti katika swalah ya Tarawiyh waigiliza kisomo cha Qur-aan cha wengine kwa sababu ya kuboresha sauti zao. Je, kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah na kinafaa?

Jibu: Kusoma Qur-aan kwa sauti nzuri ni jambo limewekwa katika Shari´ah ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameliamrisha. Usiku mmoja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisikia kisomo cha Abu Muusa al-Ash´ariy ambapo akapendekezwa na kisomo chake mpaka akamwambia:

“Umepewa moja katika sauti nzuri kabisa za Daawuud.”[1]

Kujengea juu ya haya imamu wa msikiti akimwigiliza mtu ambaye ana sauti na kisomo kizuri ili apate kuboresha sauti na kisomo chake cha Qur-aan, basi hakika jambo hilo limesuniwa kwa dhati yake na pia limesuniwa kwa sababu nyenginezo. Kwa sababu kufanya hivo kunawachangamsha waswaliji nyuma yake na sababu ya kuzihudhurisha nyoyo zao na kumsikiliza na kunyamaza kwa ajili ya kisomo chake. Fadhilah za Allaah humpa amtakaye na Allaah ni Mwenye fadhilah kuu.

[1] al-Bukhaariy (5048) na Muslim (793).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 25
  • Imechapishwa: 20/04/2021