26. Hospitali inaagiza madawa kwenda kwenye hospitali nyingine

Swali 26: Ni ipi hukumu kwa ambaye anachukua dawa kutoka kwenye duka la madawa ambayo anayasimamia yeye na anayaagiza kwenda kwa wagonjwa wengine kwenye hospitali nyingine au nyumbani kwa hoja kwamba ni muislamu na madawa hayo si ya kuuzwa?

Jibu: Mambo haya yana nidhamu na maelekezo yake. Ikiwa duka la madawa ni kwa ajili ya hospitali maalum basi madawa yasitumiwe kwa wagonjwa na wahusika wengine. Kwa sababu hospitali hii ina wahusika wake. Kwa hivyo ni wajibu kuyatumia madawa ya dula la madawa lililotajwa juu yao na yasiagizwe kwenda kwenye hospitali nyingine. Kila hospitali ina dula la madawa yake. Kwa hivo yasitolewe madawa kwenye duka moja kwenda kwengine. Kwa sababu hayo ndio maelekezo kutoka serikalini. Ikiwa dula la madawa wana maelekezo kutoka katika wizara ya afya yanayoruhusu kuagiza madawa kwenda kwenye hospitali nyingine, hakuna neno. Vinginevyo ni lazima kutii maelekezo na mtu asizidishe juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 12/10/2019