26. Hayaa na uchache wa kuzungumza

117 – Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-´Awaam bin Hawshab ametueleza, kutoka kwa Abu Swaadiq, kutoka kwa´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Hakika imani ina sehemu tatu: imani, swalah na mkusanyiko. Swalah haikubaliwi pasi na imani. Mwenye kuamini, basi huswali. Mwenye kuswali, hushikana na mkusanyiko. Yule mwenye kutengana na mkusanyiko kiasi cha shibiri, basi ameng´oa kitanzi cha Uislamu kutoka shingoni mwake.”[1]

118 – Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Muhammad bin Mutwarrif ametueleza, kutoka kwa Hassaan bin ´Atwiyyah, kutoka kwa Abu Umaamah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hayaa na kutokusema[2] ni tanzu mbili za imani.”[3]

[1] Cheni ya wapokezi ni yenye kukatika kati ya Abu Swaadiq na ´Aliy, kama ilivyo katika ”at-Taqriyb”.

[2] Bi maana kuchunga ulimi kutozungumza uwongo. Haihusiani na kunyamaza kwa moyo, kunyamaza kwa matendo  wala kunyamaza kwa ulimi kutokana na kasoro, kama alivosema al-Munaawiy.

[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. at-Tirmidhiy ameipokea kupitia njia nyingine, kutoka kwa Yaziyd bin Haaruun, na akasema:

”Hadiyth ni nzuri na geni. Kutokusema ni uchache wa kuzungumza.”

Uzindushi imekuja katika ile ya asili baada ya Muhammad bin Mutwarrif “kutoka kwa Yaziyd”. Nikaifuta kwa sababu haipo katika ”al-Muswannaf”, at-Tirmidhiy wala kwenginepo.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 44
  • Imechapishwa: 17/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy