27. Hadiyth “Nyookeni sawasawaa ingawa hamtoweza yote ipasavyo…. “

379 – Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

استقيموا ولن تُحصوا، واعلموا أنَّ خيرَ أعمالِكم الصلاةُ، ولن يحافظَ على الوُضوءِ إلا مؤمن

“Nyookeni sawasawa ingawa hamtoweza yote ipasavyo. Tambueni kuwa bora ya matendo yenu ni swalah. Hakuna anayechunga wudhuu´ isipokuwa muumini.”[1]

Ameipokea al-Haakim, ambaye amesema:

“Ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Haina kasoro isipokuwa mawazo (وهم) ya Abu Bilaal.”

Ibn Hibbaan amepokea kama hiyo katika “as-Swahiyh” yake kupitia njia nyingine isipokuwa ya Abu Bilaal. Imekwishatangulia katika mlango “Mahimizo ya kuhifadhi wudhuu´”.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/275)
  • Imechapishwa: 17/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy