8 na 9- Kufa kwa kuzama na kwa kuangukiwa na jengo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna aina tano ya mashahidi; mwenye kufa kwa tauni, mwenye kufa kwa maradhi ya tumbo, mwenye kuzama, mwenye kufa kwa kuangukiwa na jengo na shahidi katika njia ya Allaah.”

Ameipokea al-Bukhaariy (06/33-34), Muslim (06/51), at-Tirmidhiy (02/159), Ahmad (02/352,533) kupitia kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 53
  • Imechapishwa: 02/02/2020