7- Kufa kwa ugonjwa wa tumbo. Kuhusu hilo kuna Hadiyth mbili:

A-  “… mwenye kufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi.”

Ameipokea Muslim na wengineo. Imekwishatangulia kwa ukamilifu wake katika “alama ya tano”.

B- ´Abdullaah bin Yasaar amesimulia:

“Nilikuwa nimekaa pamoja na Sulaymaan bin Swurad na Khaalid bin ´Urfutwah wakataja kwamba kuna mtu amekufa kwa maradhi ya tumbo lake. Tahamaki wawili hao wakatamani wawe miongoni mwa wale wataoshuhudia (swalah ya) jeneza yake. Mmoja wao akamwambia mwengine: “Je, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si amesema:

“Yule mwenye ambaye tumbo lake litamuua hatoadhibiwa ndani ya kaburi?” Akasema: “Ndio.”

Katika upokezi mwingine:

“Umesema kweli.”

Ameipokea an-Nasaa´iy (01/289), at-Tirmidhiy (02/160) ambaye ameifanya kuwa nzuri. Vilevile ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (728) – al-Mawaarid), at-Twayaalisiy (1288), Ahmad (04/262) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 53
  • Imechapishwa: 02/02/2020