Enyi waislamu! Tunawakumbusha ubora wa mwezi huu mtukufu na tunamuomba Allaah atuwezeshe kuutumia muda wake kwa matendo mema, atukubalie na atusamehe makosa yetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujibu. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kila tendo la mwanaadamu hulipwa kwa wema mara kumi hadi mara mia saba.” Allaah (Ta´ala) amesema: ”Isipokuwa swawm, kwani hiyo ni Yangu na Mimi ndiye ninailipa. Ameacha matamanio yake, chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu. Kwa mwenye kufunga kuna furaha mbili: furaha wakati wa kufungua na furaha wakati wa kukutana na Mola wake. Harufu ya mdomo wa mwenye kufunga mbele ya Allaah ni bora zaidi kuliko harufu ya miski.”[1]
Hadiyth hii Tukufu inafahamisha fadhilah na sifa nyingi za swawm miongoni mwa ´ibaadah nyingine.
Miongoni mwa fadhilah hizo ni kwamba kuzidishiwa thawabu zake kunatofautiana na matendo mengine, kwani thawabu za swawm hazina kikomo maalum ilihali matendo mengine hulipwa wema mara kumi hadi mara mia saba.
Miongoni mwa fadhilah zake ni kwamba utakasaji wa nia katika funga ni mkubwa zaidi kuliko ´ibaadah nyingine, kwa sababu ya maneno yake:
”Ameacha matamanio yake, chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu.”
Miongoni mwa fadhilah zake ni kwamba Allaah ameitenga swawm kwa ajili Yake peke Yake miongoni mwa matendo yote na Yeye ndiye Mwenye kumlipa mfungaji, kama ilivyokuja katika maneno yake:
”Swawm ni kwa ajili Yangu na Mimi ndiye ninailipa.”
Miongoni mwa fadhilah zake pia ni kupata furaha kwa mwenye kufunga duniani na Aakhirah. Furaha ya duniani ni wakati wa kufungua kwa kile alichomhalalishia Allaah na furaha ya Aakhirah ni kwa yale aliyomwandalia Allaah katika thawabu kubwa, jambo ambalo ni furaha yenye kusifiwa kwa kuwa ni furaha ya kumtii Allaah. Amesema (Ta´ala):
قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا
“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Zake, basi kwa hayo wafurahi.”[2]
[1] al-Bukhaariy (1894), (1904) na Muslim (1151).
[2] 10:58
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 28-29
- Imechapishwa: 17/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 28-29
Imechapishwa: 17/02/2026
https://firqatunnajia.com/25-miongoni-mwa-fadhilah-za-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket