25. Maneno ya Salmaan al-Faarisiy kuhusu mikono ya Allaah

26- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Salmaan al-Faarisiy ambaye amesema:

“Allaah aliuvimbisha udongo wa Aadam kwa nyusiku arubaini kisha akaukusanya mkononi Mwake. Baadaye akatoa nje vizuri vyote kwa mkono Wake wa kuume na vibaya vyote kwa mkono Wake wa kushoto.”[1]

Hammaad bin Salamah akaashiria kwa mkono wake. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Hammaad akafuta kwa mkono wake mmoja juu ya mwingine na hivyo ndivo alivofanya Hajjaaj al-A´war. Hajjaaj ameyapokea haya kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Sulaymaan at-Taymiy, kutoka kwa Abu ´Uthmaan an-Nahdiy, kutoka kwa Salmaan.

[1] al-Bayhaqiy (2/153), Abuush-Shaykh (1006) na Ibn Mandah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” (484).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 23
  • Imechapishwa: 27/06/2019