24. Dalili ya kumi na nne kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

24- Imepokelewa kwa cheni ya wapokezi nzuri kwenda kwa Ibn ´Umar ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaishika kwa mkono Wake wa kuume na mikono Yake miwili yote ni ya kuume. Akaandika [mambo ya] kidunia na kila kitachopitika ndani yake.”[1]

Ameipokea Baqiyyah bin al-Waliyd kutoka kwa Artwa-ah bin al-Mundhir, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Umar.

[1] Ibn Abiy ´Aaswim (106) na al-Aajurriy, uk. 175

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 23
  • Imechapishwa: 27/06/2019