26. Maneno ya Ibn ´Abbaas kuhusu mikono ya Allaah

27- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) alitoa kizazi cha Aadam kutoka mgongoni mwake kama mfano wa waduduchungu na akasema: “Ee fulani! Fanya kadha! Ee fulani! Fanya kadha!” Kisha akashika kwa kukamata mara mbili, mkamato mmoja kwa mkono Wake wa kuume na mkamato mwingine mwingine kwa mkono Wake mwingine. Akasema kuwaambia wale walioko mkononi Mwake wa kuume: “Ingieni Peponi!” na Akasema kuwaambia wale walioko kwenye mkono Wake mwingine: “Ingieni Motoni na wala sijali!”[1]

Ameipokea al-A´mash, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas.

[1] Ibn Mandah katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (29) na Ibn Battah katika ”al-Ibaanah” (1614) na (1633).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 24
  • Imechapishwa: 27/06/2019