Malengo na makusudio ya ulinganizi ni kuwatoa watu katika giza na kuwapeleka katika nuru na kuwaelekeza katika haki ili waitendee kazi na wasalimike kutokana na Moto, wasalimike kutokana na ghadhabu za Allaah. Vilevile kumtoa kafiri kutoka katika giza la ukafiri na kumwingiza katika nuru na uongofu. Aidh kumtoa mjinga kutoka katika giza la ujinga na kumwingiza katika nuru ya elimu na mtenda dhambi kutoka katika giza la maasi na kumwingiza katika nuru ya utiifu. Haya ndio malengo ya ulinganizi. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ

“Allaah ni mlinzi wa wale ambao wameamini; Anawatoa kutoka katika viza na  kuwaingiza katika nuru. ”[1]

Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wametumwa ili wawatoe watu kutoka katika giza na kuwapeleka katika nuru. Vivyo hivyo walinganizi wa haki wanasimamia kazi ya ulinganizi na wana uchangamfu kwayo ili kuwatoa watu kutoka katika giza na kuwaingiza katika nuru, kuwaokoa kutokana na Moto na kumtii shaytwaan na kuwaokoa kutii matamanio na kumtii Allaah na Mtume Wake.

[1] 02:257

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 14/06/2023