25. Kuchelewesha kulipa mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine

Akichelewesha kulipa mpaka akafikiwa na Ramadhaan nyingine, basi atafunga Ramadhaan ya sasa na atafunga zile siku anazodaiwa baadaye. Jengine ni kwamba akiwa alichelewesha kutokana na udhuru uliomfanya asiweze kulipa katika kipindi hicho, basi hakuna kinachomlazimu isipokuwa kulipa tu. Akiwa alichelewesha pasi na udhuru, basi – mbali na kulipa – atamlisha masikini nusu ya Swaa´ ya chakula kilichozoeleka katika mji kwa kila siku moja iliyompita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/388)
  • Imechapishwa: 05/04/2021