4 – Inafaa kwa mfungaji kumwaga maji juu ya kichwa chake kwa ajili ya kupata kibaridi kidogo na pia inafaa akasukutua mdomo. Abu Daawuud amepokea kupitia Hadiyth ya mmoja katika Maswahabah:
“Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huko al-´Arj akijimwagia maji juu ya kichwa chake kutokana na kiu au joto kali ilihali amefunga.”[1]
[1] Abu Daawuud (2365).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 43
- Imechapishwa: 22/04/2023