La pili: Kipindi cha Ilaa´ kiko pamoja na hedhi na si nifasi. Ilaa´ maana yake ni mume kuapa kuwa hatofanya jimaa na mke wake kabisa au chini chini miezi mine. Akifunga kiapo hicho na mke akamtaka wafanye jimaa ambapo akakataa, ana miezi mine kuanzia ile siku alipofunga kiapo. Baada ya muda kutimia atalazimika kufanya naye jimaa. La sivyo mke ataomba talaka. Ikiwa ndani ya muda huu atapata nifasi, muda huu hauhesabiki kwa mume. Miezi mine hiyo itakuwa ni ya kipekee pasi na nifasi. Tofauti na hedhi ambayo miezi mine hiyo itahesabika kwa mume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016