Hukumu za nifasi ni zile zile kama hukumu za hedhi isipokuwa katika mambo yafuatayo:

La kwanza: Eda inaisha kwa kuzaa na sio kwa nifasi. Talaka ikipitika kabla ya kuzaa basi eda inaisha kwa kuzaa na si kwa nifasi. Na ikiwa talaka itapitika baada ya kuzaa, basi itabidi asubiri mpaka pale atapopata hedhi halafu aangalizie hapo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016