Kwa hakika mungu kwa mujibu wao ni yule ambaye anakusudiwa [anayeombwa] kwa ajili ya mambo haya, sawa ikiwa ni Malaika, Mtume, walii, mti, kaburi au jini.

MAELEZO

Hii ni sababu ya yale yaliyotangulia katika kuthibitisha maana ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` na kwamba ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Kwa kuwa mungu kwa mujibu wa waarabu ni yule anayeabudiwa kwa ajili ya kutatua mahitajio na kuondosha matatizo na huzuni. Mungu kwa mujibu wao hakuwa yule mwenye kuumba, kuruzuku na kuyaendesha mambo. Hawakuwa wanaonelea kuwa huyu ndiye mungu wao. Shirki kwao haikutokea katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, bali ilitokea katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 39
  • Imechapishwa: 07/11/2016