Ambaye atakula ndani ya Ramadhaan kutokana na sababu inayokubalika katika dini (kama mfano wa zile nyudhuru za kidini ambazo zinamhalalishia yeye kula) au kwa sababu za haramu (kama mfano wa ambaye anaiharibu funga yake kwa kufanya jimaa au kitu kingine), basi atalazimika kulipa. Amesema (Ta´ala):
فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ
“Akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[1]
Inapendekeza kuharakisha kulipa kwa ajili ya kutakasa dhimma yake. Pia inapendeza mtu alipe kwa kufuatanisha. Kwani kulipa kunasimulia kutekeleza. Asipolipa papohapo basi anatakiwa kuazimia kufanya hivo. Inafaa kwake kuchelewesha kwa sababu wakati wake ni wenye wasaa. Kila jambo la wajibu ambao umewekewa muda wenye wasaa inafaa kulichelewesha sambamba na kuliazimia. Aidha inafaa kufunga masiku mbalimbali. Lakini kusipobaki kufika kwa Sha´baan isipokuwa kwa kiwango cha yale masiku anayodaiwa, basi katika hali hiyo analazimika kuyafululiza yote kutokana na ufinyu wa wakati. Haijuzu kuchelewesha mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine pasi udhuru. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Nilikuwa nikidaiwa funga ya Ramadhaan na siwezi kuilipa isipokuwa ndani ya Sha´baan. Hili ni kutokana na ile nafasi yangu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]
Hiyo imejulisha kuwa wakati wa kulipa ni wenye wasaa mpaka pale kutapobaki katika Sha´baan isipokuwa kile kiwango cha masiku anayodaiwa. Hapo atalazimika kuyafunga kabla ya kuingiliwa na Ramadhaan mpya.
[1] 02:184
[2] al-Bukhaariy (1950) na Muslim (2682).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/387-388)
- Imechapishwa: 05/04/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
06. Kufunga deni la Ramadhaan
03 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia: “Nilikuwa na deni la swawm ya Ramadhaan na siwezi kuilipa isipokuwa katika Sha´baan.”[1] Kuna maafikiano juu yake. Hadiyth inajulisha kuwa ambaye amekula katika Ramadhaan kutokana na udhuru kwamba analazimika kulipa na kwamba si lazima kulipa kwa haraka. Bali ulazima wake unaweza kucheleweshwa. Inafaa…
In "02. Hadiyth baada ya Ramadhaan"
43. Ulazima wa kulipa siku zilizompita mtu Ramadhaan
Kila ambaye imefaa kwake kuacha kufunga kutokana na moja ya sababu zilizotangulia basi hakemewi kwa kula kwake hadharani waziwazi ikiwa sababu yake ni yenye kuonekana kama mfano wa mgonjwa na mzee asiyeweza kufunga. Lakini sababu ya kutokufunga kwake ikiwa ni yenye kujificha, kama mfano wa mwenye hedhi na mwenye kumwokoa…
In "Majaalis Shahr Ramadhwaan - Ibn ´Uthaymiyn"
21. Baadhi ya hukumu kuhusu kulipa deni la Ramadhaan
Mlango wa nne: Kulipa, swawm iliyopendekezwa, yaliyochukizwa na kuharamishwa wakati wa kufunga. Ndani yake kuna masuala yafuatayo: Suala la kwanza: Kulipa funga Mtu akila siku miongoni mwa siku za Ramadhaan basi ni lazima kwake kutubu kwa Allaah na amwombe msamaha. Kwa sababu hiyo ni jarima na dhambi kubwa. Pamoja na…
In "1. Suala la kwanza: Kulipa funga"