24. Haifai kuwakufurisha mayahudi na manaswara kwa sababu wamefikiwa na Uislamu kwa sura mbaya?

Swali 24: Yeyote ambaye anasema:

“Mayahudi na manaswara wamefikiwa na ulinganizi wa Kiislamu kwa sura mbaya na kwa ajili hiyo hatuwakufurishi.”

Ni ipi hukumu ya maneno haya?

Jibu: Si sahihi. Bali wamefikiwa na ulinganizi tangu wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye mwenyewe aliwafikishia, Maswahabah pia waliwafikishia, walinganizi waliwafikishia na maimamu waliwafikishia. Hata Shaykh-ul-Islaam aliwafikishia wenyewe. Hivyo kusema kwamba hawakufikiwa na ujumbe ni batili.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 56
  • Imechapishwa: 09/01/2026