Anashirikiana na mabenki ya ribaa kwa hoja eti hachukui faida

Swali: Mtu anashirikiana na mabenki ya ribaa na alipoulizwa kwa nini anashirikiana na mabenki hayo akasema kwamba yeye hachukui faida za ribaa.

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wale wanaokula ribaa, wanaowahusisha nayo, waandishi wake na mashahidi wake na akasema:

“Wote hawa ni sawa.”

Hivyo kushirikiana na wale wanaoshughulika na ribaa au kufanya biashara nayo haijuzu, kwa sababu Allaah amesmea:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى

“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah.”[1]

Kwa hiyo muislamu haipaswi kushiriki katika biashara zinazohusisha ribaa.

[1] 05:02

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2425/حكم-من-يتعامل-مع-البنوك-الربوية-دون-اخذ-الفاىدة
  • Imechapishwa: 09/01/2026