Mlango

Miongoni mwa yanayofahamisha maana ya maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.”[1]

45 – Muhammad bin Sa´iyd bin Ishaaq ametukhabarisha: ´Amr bin Sa´iyd al-Jammaal ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Abdillaah bin Mas´uud ametuhadithia: Abul-Waliyd ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Murrah: Nimemsikia Abu ´Ubaydah amesimulia kutoka kwa Abu Muusa al-Ash´ariy, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) hunyoosha mkono Wake mchana ili atubie aliyekosea usiku, mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.”[2]

46 – Muhammad bin ´Abdillaah bin Abiy Rajaa’ ametukhabarisha huko Makkah: Muusa bin Haaruun ametuhadithia: Muhammad bin as-Sabbaah ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Haazim ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Muqsim, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema juu ya mimbari:

”al-Jabbaar atazichukua mbingu Zake na ardhi Yake kwa mkono Wake, azikamate, aukunje na kuunyosha na kusema: ”Mimi ni al-Jabbaar! Mimi ni Mfalme! Wako wapi wenye jeuri? Wako wapi wenye kufanya kiburi?”[3]

Hadiyth hii imethibiti kwa maafikiano.

47 – ´Abdur-Rahmaan bin Yahyaa bin Mandah na ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Muqriy wametukhabarisha: Abu Mas´uud Ahmad bin al-Furaat ametuhadithia: ´Aliy bin Ishaaq ametuzindua: Ibn-ul-Mubaarak ametuhadithia: Yuunus ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah ataikamata ardhi siku ya Qiyaamah, atazikunja mbingu kwa mkono Wake wa kuume na kusema: ”Mimi ni Mfalme! Wako wapi wafalme wa ardhini?”[4]

48 – ´Abdullaah bin Ibraahiym ametukhabarisha: Abu Mas´uud ar-Raaziy ametuhadithia: ´Aliy bin Ishaaq ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-ul-Mubaarak, kutoka kwa ´Anbasah, kutoka kwa Habiyb bin Abiy ´Amrah, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye amesema:

”Nilimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu maneno Yake (Jalla wa ´Azz):

وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”… ardhi yote itawekwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[5]

”Watu watakuwa wapi kipindi hicho?” Akasema: ”Juu ya Njia.”[6]

[1] 5:64

[2] Muslim (2113).

[3] Muslim (2149).

[4] al-Bukhaariy (4812).

[5] 39:67

[6] at-Tirmidhiy (3241), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri, Swahiyh na geni. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3241).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 74-76
  • Imechapishwa: 16/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy