22. Watakuwa upande wa mkono wa kuume wa Mola

44 – al-Hasan bin Muhammad bin an-Nadhwr ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Yaziyd ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar al-Makkiy, kutoka kwa ´Amr bin Aws, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru upande wa mkono wa kulia wa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) na mikono Yake yote ni ya kuume; ni wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao, familia zao na yale wanayoyasimamia.”[1]

Hadiyth hii imethibiti kwa maafikiano.

[1] Muslim (1827).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 73
  • Imechapishwa: 16/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy