23. Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ndio maana ya Shahaadah

Maana ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` ndio Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na sio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Iwapo maana yake ingelikuwa ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asingeliwaambia washirikina:

“Semeni ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah´.” Ahmad (03/492).

Kwa sababu wao walikuwa wakisema Allaah kuwa ndiye Muumbaji, Mruzukaji, Muhuishaji na Mfishaji na hapo ndipo anataka kuwafikisha kwenye malengo na anawapiga vita kwa kitu ambacho wanakitambua na kukikubali. Haya ni maneno batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 38
  • Imechapishwa: 07/11/2016