Ni kina nani walimwengu? Jibu mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu [kimeumbwa] na mimi ni mmoja katika walimwengu hao.”

Mimi na wewe pia tunaingia katika walimwengu hao. Mbingu ni walimwengu, ardhi ni walimwengu, majini ni walimwengu, watu ni walimwengu, Malaika ni walimwengu, miti ni walimwengu na bahari ni walimwengu. Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu. Walimwengu wote hawa – walimwengu walioko juu na walimwengu walioko chini – Mola wake ni Allaah. Kinachofahamisha juu ya hilo ni maneno ya Muusa wakati Fir´awn alipomuuliza:

قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ

“Fir’awn akasema: “Kwani ni nani Mola wa walimwengu?” Akasema: “Mola wa mbingu na ardhi na yaliyomo baina yake mkiwa ni wenye yakini.””[1]

Imepokelewa kutoka kwa Mujaahid, al-Hasan na Qataadah ya kwamba ni viumbe wote[2]. al-Qurtwubiy amenukuu maneno ya Qataadah ya kuwa ni kila asiyekuwa Allaah[3]. az-Zajaaj – ambaye ni mwanachuoni wa lugha – amesema ni kila alichoumba Allaah[4] na katika maneno ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah[5] na Ibn Kathiyr[6]. Ama kuhusu walimwengu waliokusudiwa katika maneno Yake (´Azza wa Jall):

لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“… ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”[7]

ni watu na majini. Neno walimwengu ndani ya Qur-aan lina maana nyingi. Ni kama ambavo neno ummah ndani ya Qur-aan lina maana nyingi.

[1] 26:23-24

[2] Tafsiyr-ul-Baghawiy (01/52).

[3] Tafsiyr-ul-Qurtwubiy (01/138).

[4] Ma´aaniy al-Qur-aan wa I´raabih (01/46).

[5] Talbiys-ul-Jahmiyyah (04/168, 397) na ”Dar’ Ta´aarudhw-il-´Aql wan-Naql” (01/125).

[6] Tafsiyr Ibn Kathiyr (01/131).

[7] 25:01

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 06/02/2023