Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
… na huenda amelisema huku akidhania ya kwamba yanamkurubisha kwa Allaah, kama walivyodhania washirikina. Na khaswa Allaah akikuongoza kwa yale aliyoelezea kuhusu watu wa Muusa (´alayhis-Salaam) – pamoja na wema wao na elimu yao – walipomuendea na kumwambia:
اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ
”Tufanyie nasi mungu kama walivokuwa hawa wana miungu!” (07:138)
Hapo ndipo khofu na bidii yako itaongezeka na yatakayokuokoa kutokana na haya mfano wake.
MAELEZO
Wakati Shaykh (Rahimahu Allaah) alipotahadharisha juu ya mambo mawili – ambapo moja wapo khofu ya mtu kwa kufikiria kuwa Tawhiyd maana yake ni kuamini kuwa Allaah (Ta´ala) peke Yake ndiye muumbaji, mwenye kutoa riziki na mwenye kuyaendesha mambo – anabainisha mtu anatakiwa siku zote kuwa na khofu. Kisha akataja watu wa Muusa waliomwambia:

”Tufanyie nasi mungu kama walivokuwa hawa wana miungu!”
Amewabainishia kuwa maombi yao kufanyiwa mungu kama jinsi wale wengine walivyokuwa na mungu, ilikuwa inatokamana na ujinga. Hili linapelekea mwanadamu awe na khofu juu ya nafsi yake, ili asije kutumbukia katika upotevu na ujinga kwa njia ya kwamba akafikiria kuwa “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” maana yake ni hakuna mwenye kuumba, mwenye kuruzuku na mwenye kuyaendesha mambo isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall).
Haya ambayo Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema na kutahadharisha wametumbukia ndani yake wanafalsa wengi. Wamezungumzia juu ya Tawhiyd na kusema kuwa “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” maana yake ni hakuna mwengine zaidi ya Allaah mwenye kuumba na hakuna mwengine zaidi ya Allaah mwenye uwezo wa kuumba. Hivyo wakafasiri maneno haya makubwa kwa njia batilifu. Hakuna muislamu aliyefahamu namna hii. Bali hata makafiri hawakufahamu namna hii. Uhakika wa mambo ni kwamba hata wale washirikina ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa kwao walikuwa wakifahamu maana ya maneno haya bora zaidi kuliko hawa wanafalsafa.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 46-47
- Imechapishwa: 14/10/2023

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 46-47
Imechapishwa: 14/10/2023
https://firqatunnajia.com/23-mlango-wa-04-ufahamu-mbaya-wa-shahaadah-ni-upotevu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)