Amesema kumwambia Muusa:

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

”Mimi Niko pamoja nanyi; Nasikia na naona.”[1]

Maeneo mengine amesema:

إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ

”Hakika Sisi tuko pamoja nanyi Wenye kusikiliza.”

Wanahoji kwa kusema ni vipi anaweza kusema:

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”[2]

na katika Aayah nyingine anasema:

إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ

”Hakika Sisi tuko pamoja nanyi Wenye kusikiliza.”

Wakaitilia shaka Qur-aan kwa sababu hiyo.

Kuhusu maneno Yake:

إِنَّا مَعَكُم

”Hakika Sisi tuko pamoja nanyi… ”,

hivo ni kutokana na mafumbo ya lugha. Mtu anaweza kumwambia mwenzie ”Sisi tutakulipa riziki yako” na ”Sisi tutakufanyia kadhaa na kadhaa”. Kuhusu maneno Yake:

إِنَّنِي مَعَكُمَا

”Hakika Mimi niko pamoja nanyi… ”

Kilugha ni jambo la sawa ambapo mtu anaweza kumwambia mwenzie ”Nitakulipa riziki yako” na ”Nitakufanyia kadhaa na kadhaa”[3].

[1] 20:46

[2] 57:4

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 22/04/2024