Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

ولا تقل القرآن خلْقٌ قرأْتُهُ

05 – Wala usiseme kuwa kisomo cha Qur-aan kimeumbwa

فإن كلام اللهِ باللفظ يُوضحُ

     kwani hakika maneno ya Allaah yanawekwa wazi kwa matamshi

MAELEZO

Haya ni madhehebu ya tatu katika masuala haya.

1 – Wanasema wazi kuwa Qur-aan ni kiumbe.

2 – Wanasimama. Bi maana hawasemi kuwa imeumbwa wala haikuumbwa.

3 – Matamshi ya Qur-aan ni kiumbe. Mtu anasema kuwa matamshi yake ya Qur-aan yameumbwa. Hii ni njama ya kusema kuwa Qur-aan imeumbwa. Haijuzu kwako kusema kuwa matamshi yako ya Qur-aan yameumbwa na wala haijuzu vilevile kusema kuwa matamshi yako ya Qur-aan hayakuumbwa. Ni lazima upambanue. Kwa sababu ukisema kwamba matamshi yako ya Qur-aan ni kiumbe na usipambanue, hii ni ´Aqiydah ya Jahmiyyah. Vilevile ukisema kuwa matamshi yako ya Qur-aan sio kiumbe, huku ni kuwasapoti ´Aqiydah ya Jahmiyyah. Kwa kuwa ukisema kwamba matamshi yako ya Qur-aan hayakuumbwa, utakuwa umeingiza matendo yako pamoja na matendo ya Allaah na umefanya kitendo chako hakikuumbwa. Hii ni ´Aqiydah ya Qadariyyah ambao wanapinga makadirio na wanaona kuwa viumbe ndio wanaovumbua na kuumba matendo yao wenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 75
  • Imechapishwa: 02/01/2024