23. Matamshi na kile chenye kutamkwa

Kipengele hichi pia kitahusiana na Qur-aan.

Imeshatangulia ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Lakini hata hivyo ni sahihi kusema kuwa matamshi ya Qur-aan yameumbwa au hayakuumbwa au ni wajibu kunyamazia hilo?

Si sahihi kuthibitisha au kukanusha jambo hili kwa njia ya kuachia. Lakini ikiwa mtu kwa matamshi anakusudia maneno ambacho ni kile kitendo cha msomaji, yameumbwa. Mja ameumbwa yeye pamoja na kitendo chake. Ikiwa mtu matamshi anakusudia kile chenye kutamkwa, basi ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Kwa sababu maneno ya Allaah ni moja katika sifa Zake na sifa Zake hazikuumbwa. Ufafanuzi huu unaashiriwa na Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) pale aliposema:

“Mwenye kusema matamshi ya Qur-aan yameumbwa na huku akilenga Qur-aan, basi huyo ni Jahmiy.”

Ina maana ya kwamba ikiwa hakusudii Qur-aan yenyewe, isipokuwa anakusudia yale matamshi ambayo ni kitendo cha msomaji mwenyewe, basi si Jahmiy – na Allaah ndiye mwenye kujua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 65
  • Imechapishwa: 07/05/2020