21 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipohukumu viumbe aliandika katika kitabu Chake kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: ”Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[1]
Imekuja Katika tamko jengine:
“Allaah kabla hajaumba viumbe aliandika kitabu: “Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.” Kiko Kwake juu ya ´Arshi.”
Imekuja Katika tamko jengine:
”Wakati Allaah alipoumba viumbe, aliandika kitabu juu yake Mwenyewe. Kimenyanyuliwa juu ya ´Arshi: “Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (3194), Muslim (2751), Ahmad (2/466) na wengineo.
[2] Hadiyth ni Swahiyh. Baadhi ya matamshi yake yapo kwa al-Bukhaariy na Muslim. Tamko la mwisho liko kwa at-Tirmidhiy. Nimeitaja katika “as-Swahiyhah” (1629) na ”Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (810-811).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 92
- Imechapishwa: 12/04/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
20. Dalili ya kumi na nane kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe
18- Abul-Fath bin al-Battwiy ametuhathia: Abul-Fadhl bin Khayruun ametuhathia: Abu ´Aliy bin Shaadhaan ametuhathia: Abu Sahl bin Ziyaad ametuhathia: al-Qaadhwiy Ahmad bin Muhammad al-Bartwiy ametuhathia: al-Qa´nabiy ametuhathia: al-Mughiyrah bin ´Abdir-Rahmaan al-Qurashiy ametuhathia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swall Allaahu…
In "Ithbaatu Swifat-il-´Uluww"
87. Kitabu kilichoko kwa Allaah
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh: “Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipohukumu viumbe aliandika katika kitabu Chake kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: ”Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[1] MAELEZO Hadiyth inafahamisha kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi. ´Arshi ndio…
In "at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah"
12. Dalili ya kwamba Allaah yuko juu ya mbingu
12- Muhammad bin Ahmad al-Haakim (Rahimahu Allaah) ametuhadithia: Muhammad bin Muhammad al-Anmaatwiy ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Husayn al-Kisaa-iy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Yahyaa al-Madaniy ametuhadithia: Maalik ametuhadithia, kutoka kwa ´Abuu-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Pindi Allaah (´Azza…
In "al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd"