20 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati Allaah anapompenda mja, basi humwita Jabraaiyl na kusema: “Hakika Mimi nampenda mja Wangu; nanyi pia mpendeni!” Jabraaiyl akawaeleza hilo wabebaji wa ´Arshi na wakazi wa mbinguni husikia kishindo cha ´Arshi ambapo wakazi wa mbingu ya saba wakampenda. Kisha ikaenda mbingu baada ya mbingu mpaka ikafika katika mbingu ya chini. Halafu ikashuka mpaka ardhini na akapendwa na watu wa ardhini.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh na yenye kuthibiti.

Maoni yetu juu ya Hadiyth hizi ni kwamba tunaamini zile zilizosihi na yale ambayo wameafikiana juu yake Salaf katika kuzipitisha na kuzikubali Kuhusu zile ambazo kwenye cheni ya wapokezi wake kuna kasoro na ambazo Salaf wamekinzana juu ya kukubalika kwake na maana yake, hatuthibitishi chochote. Bali tunazipokea kwa jumla na tunabainisha hali yake. Tumeitaja Hadiyth hii kutokana na kule kupokelewa kwake kwa wingi juu ya uwepo wa Allaah (Ta´ala) juu ya ´Arshi Yake na pia inaafikiana na Aayah za Qur-aan.

[1] al-Bukhaariy, Muslim na at-Tirmidhiy mfano wake, kwa kifupi. Imetajwa katika “adh-Dhwa´iyfah” (2207).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 91-92
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy