19 – Ibn ´Abbaas amesimulia kuwa baadhi ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walimweleza:

”Wakati walipokuwa wamekaa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ilianguka nyota yenye kung´ara. Akasema: ”Ni kipi mlikuwa mnasema wakati kunapoanguka kitu kama hiki?” Wakasema: ”Tulikuwa tukisema kuna mtu mkubwa amezaliwa au amekufa hii leo.” Akasema: ”Haianguki kwa kufa au kuishi mtu, basi Mola wetu (´Azza wa Jall) anapohukumu jambo, basi husabihi wale wabebaji wa ´Arshi mpaka wale wakazi wa mbingu inayofuata nao wakaanza kusabihi mpaka matukuzo yao ikawafikia watu wa mbingu ya chini. Wale walioko wanaowafuatia wabebaji wa ´Arshi husema: ”Nini alichosema Mola wenu?” Huwaeleza Alichosema. Wale wakazi wa mbinguni huulizana wao kwa wao mpaka jambo huwafikia wale wakazi wa mbingu ya chini. Majini huiba kitu katika yale yanayosemwa na wakawafikishia wapenzi wao. Yale wanayofikisha kwa uinje wake ni haki, huzua na wakaongeza.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 91
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy