Makatazo ya kufanya haraka kwa ajili ya kuwahi Rak´ah

Swali: Makatazo ya kuharakia swalah na kulazimiana na utulivu na upole.

Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba haya ni makatazo ya machukizo. Muumini anatakiwa kujipamba kwa adabu alizobainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Wako ambao wamefunganisha makatazo ya kukimbia wakati kunapokimiwa swalah na kwamba asifanye haraka kwa hali zote au jambo hilo ni pale tu kunapokimiwa swalah tu?

Jibu: Asifanye haraka kabisa; si wakati kunapokimiwa wala nyakati zingine. Atembee kwa utulivu.

Swali: Je, jambo hilo sio maalum kwa ajili ya ijumaa?

Jibu: Hakuna umaalum wa chochote.

Swali: Vipi mtu kufanya haraka kwa ajili ya kuwahi Rak´ah ya mwisho?

Jibu: Haijalishi kitu. Akiikosa ataikidhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23711/حكم-الاسراع-في-المشي-الى-الصلاة
  • Imechapishwa: 12/04/2024