23. Hivi ndivo wanavoamini Waaqifah na Lafdhwiyyah

Waaqifah. Ni wale wanaosema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na sambamba na hilo wanajizuilia kusema kuwa haikuumbwa. Wao ni miongoni mwa aina mbaya na ovu kabisa.

Lafdhwiyyah. Ni wale wanaosema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah lakini matamsi yake na kisomo chake kimeumbwa. Nao ni Jahmiyyah watenda maovu wakubwa.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 81
  • Imechapishwa: 02/06/2022