22. Hivi ndivo wanavoamini Jahmiyyah

Jahmiyyah. Ni maadui wa Allaah na ndio wale wanaodai kuwa Qur-aan imeumbwa. Wanadai kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hakumzungumzisha Muusa (´alayhis-Salaam), kwamba Allaah hazungumzi na wala haongei. Vilevile wanaona kuwa Allaah hatoonekana, kwamba Hana mahali na kwamba Hana ´Ashiy wala Kursiy. Yapo mengine mengi wanayosema ambayo nachukia kuyataja. Ni makafiri, mazanadiki na maadui wa Allaah. Tahadharini nao!

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 02/06/2022