104 – Ibn Fudhwayl ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, ambaye alikuwa akiwaambia marafiki zake:

”Tembea nasi tuamini kitambo.”[1]

105 – Wakiy´ ametuhadithia: al-A´mash ametueleza, kutoka kwa Jaamiy´ bin Shaddaad, kutoka kwa al-Aswad bin Hilaal al-Muhaaribiy, ambaye ameeleza kuwa Mu´aadh amesema:

”Hebu keti basi, tuamini kitambo.”[2]

Bi maana tumtaje Allaah (Ta´ala).

106 – Abu Usaamah ametukhabarisha, kutoka kwa Mahdiy bin Maymuun, kutoka kwa ´Imraan al-Qasiyr, kutoka kwa Mu´aawiyah bin Qurrah, aliyeeleza kuwa Abud-Dardaa’ alikuwa akisema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ إِيمَانًا دَائِمًا، وَعِلْمًا نَافِعًا، وَهَدْيًا قَيِّمًاٍ

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba imani ya daima, elimu yenye manufaa na uongofu ulionyooka.”[3]

Mu´aawiyah amesema:

”Tunaona kuwa miongoni mwa imani ipo ambayo si ya daima, katika elimu ipo ambayo hainufaishi na katika uongofu upo ambao si wenye kunyooka.”

107 – Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Jaamiy´ bin Shaddaad, kutoka kwa al-Aswad bin Hilaal, ambaye amesema:

”Mu´aadh alikuwa akisema kumwambia mmoja katika ndugu zake: ”Hebu keti basi, tuamini kitambo.” Wakiketi chini, wakimtaja Allaah na kumhimidi.”[4]

108 – Abu Usaamah ametukhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin Twalhah[5], kutoka kwa Zubayd, kutoka kwa Dharr, ambaye ameeleza:

”Wakati fulani ´Umar alikuwa akishika mkono wa mtu mmoja wawili akiwaambia: ”Njoo nasi, tuzidishe imani yetu.”

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. ´Alqamah alikuwa ni Ibn Qays an-Nakha´iy al-Kuufiy; mwaminifu, imara,  mwanachuoni na mfanya ´ibaadah, mmoja katika maswahiba wa Ibn Mas´uud. Maneno hayo yanatiliwa nguvu na Athar ya Mu´aadh inayofuatia.

[2]Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

[4] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Abu ´Ubayd (20) ameyapokea kupitia kwa Sufyaan, kutoka kwa al-Jaamiy´.

[5] Alikuwa ni Ibn Muswarrif al-Yaamiy al-Kuufiy; mwaminifu na mmoja katika wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim. Vivyo hivyo kuhusu mapokezi mengine, isipokuwa Dharr bin ´Abdillaah al-Murhibiy ambaye hakumdiriki ´Umar.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 41
  • Imechapishwa: 16/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy