22. Hakuna muumini yeyote misikitini

101 – Fudhwayl bin ´Iyaadh ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Khaythamah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye amesema:

”Kuna kipindi kitafika ambapo watu wanakusanyika na kuswali misikitini na hakuna kati yao aliye muumini.”[1]

102 – Yahyaa bin Ya´laa[2] at-Taymiy ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Twalq bin Habiyb, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesema:

”Mambo matatu yakikusanyika kwa mtu basi huhisi ladha ya imani na utamu wake: Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na Mtume Wake wawe ni wenye kupendwa zaidi kwake kuliko mwingine yeyote, apende kwa ajili ya Allaah na achukie kwa ajili ya Allaah.”

Akamtaja mshirikina. 

103 – Ibn Numayr ametuhadithia: Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa al-Miswar bin Makhramah na Ibn ´Abbaas, waliosema:

”Wawili hao waliingia kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipodungwa kisu. Akasema: “Swalah!” Ndipo akasema: “Hakuna fungu kwa yeyote ndani ya Uislamu aliyepoteza swalah.” Baada ya hapo akaswali na huku jeraha lake linavuja damu. Allaah amuie radhi.”[3]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Ameipokea al-Haakim (04/442) kupitia kwa Sufyaan, kutoka kwa al-A´mash. al-Haakim na adh-Dhahabiy wote wawili wameisahihisha.

[2] Katika ile ya asili imekuja “Ibn-ul-´Alaa´”. Masahihisho yamefanywa baada ya “al-Muswannaf” na vitabu vinavyozungumzia nyasifu za wanamme. Alikuwa mwaminifu na alikuwa ni katika wanamme wa Muslim. Vivyo hivyo kuhusu wengine wote. Kuna pokezi mwingine ambao umekamilika zaidi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nao unasema:

”Mambo matatu yakikusanyika kwa mtu basi huhisi ladha ya imani: Ambaye Allaah na Mtume Wake wanapendwa zaidi kwake kuliko mwingine yeyote, ampende mtu na asimpende isipokuwa iwe ni kwa ajili ya Allaah na achukie kurudi kwenye ukafiri kama anavyochukia kutupwa ndani ya Moto.” (al-Bukhaariy na Muslim)

[3] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Maalik (1/39/51) ameipokea kupitia kwa Hishaam pasi na Ibn ´Abbaas.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 40
  • Imechapishwa: 16/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy